MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU
MAJI
Pumu: Changanya juisi ya kitunguu maji na asali halafu kunywa kiasi cha kikombe
kimoja, asubuhi na jioni. Endelea hivyo kwa muda wa mwezi mmoja.
Uvimbe wa mapafu (Pneumonia): Weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya
kifua na mgongo pamoja na kufunga kwa kitambaa, fanya hivyo kila siku kabla ya
kulala.
Maradhi ya kinafsi: Chemsha kitunguu na maganda yake, baadae mgonjwa wa
kinafsi ale, au chukua juisi ya kitunguu maji na juisi ya saladi (lettuce) na
kijiko kimoja cha asali changanya vyote ndani ya blenda saga na kisha unywe.
Saratani (Cancer): Kausha maganda ya kitunguumaji kwenye jua, yasage na
kiasi cha magamba hayo chukua magamba ya muoka (muoki, maloni, oak) halafu
yakande katika asali na chukua na uchanganye katika juisi ya karoti (carrot) na
unywe kiasi ya kijiko kimoja kwa muda wa mwezi mzima mfululizo,na baadae uvute
moshi wa kitunguu maji kabla ya kulala.
Vidonda
ya saratani: Chukua
juisi ya kitunguumaji kiasi cha kikombe,chukua na kiota (kiwawi, nettle) kamua
majani yake kiasi cha kijiko kimoja na ongezea juisi ya kitunguu na halafu
chukua hina iponde ndani yake ili ipate kuwa marhamu inayopakwa katika vidonda;
fanya hivo kila siku pamoja na kunywa juisi ya kitunguu maji iliyochanganywa na
juisi ya kiota kijiko kimoja kidogo na baada ya hapo kunywa kikombe kimoja cha
maziwa.
Mvilio wa damu (Bruise): Changanya juisi ya kitunguu maji pamoja na
kiasi cha mafuta ya kafuri, sugua mahali palipo na mvilio asubuhi na jioni.
Majipu: Saga kitunguu maji na kikaange katika mafuta ya zaituni bila ya
kuwa rangi ya manjano, paka kama marhamu na funga bendeji juu yake. Kila siku
ukibadilisha pamoja na kusafisha utokaji wa usaha umalizike, halafu utakuwa
ukitumia habasouda.
Chunusi: Chukua kitunguu maji kisha ukisage, halafu ukikande katika unga wa
ngano nzima, changanya na yai pamoja na mafuta ya simsim(ufuta) na upake usoni
asubuhi na jioni pamoja na kula kitunguu kwa sana.
Ukurutu (Eczema): Chukua juisi ya kitunguu na nanaa (mint) vipimo
sawa,tengeneza kama krimu (cream) na ujipake baadae pangusa ukurutu kwa maji ya
siki nyepesi, rudia kila siku pamoja na kujiepusha na kila kinachochea hisia.
Kula matunda,mboga na asali kwa wingi.
Saratani
ya ngozi: Chukua
juisi ya kitunguu maji, uwatu uliosagwa na salfa manjano kiasi cha robo kijiko
kidogo; tengeneza marhamu jipake kila siku. Baada ya kuosha jioni jipake mafuta
ya zaituni endelea hivyo kwa muda wa wiki.
Mgonjwa wa figo na vijiwe: Chukua kitunguu bila kukichambua, weka
na mbegu ya tende baada ya kuichoma kama
vile buni na kuisaga; halafu kila siku kula kimoja kula kimoja kwa muda wa
wiki.
Kikohozi kwa wakubwa na wadogo: Saga kitunguu kitie ndani ya kikombe cha
asali; acha kwa muda wa saa tatu (3) kisha uisafishe. Kula kiasi cha kijiko
kimoja kila baada ya chakula.
Kisukari (Diabetes): Kila siku kula kitunguu. Sukari itashuka na baadae
kula mzizi wa kabichi (cabbage).
Maradhi ya macho: Chukua maji ya kitunguu na asali vipimo sawa halafu
ujipake jichoni (kama unavyojipaka wanja) , (dawa hii naamini ni dawa bora kwa
maradhi ya macho yote nakuambuka marehemu bibi yangu alikuwa akiwatibu wagonjwa
wenye mtoto wa jicho kwa kutumia dawa hii) jipakae jichoni kwa kutumia glass
rod au kama huna kifaa hicho unaweza kutumia nyoya la kuku au ndege yoyote.
Kikohozi: Chemsha maji ya kitunguu maji na asali kunywa kijiko kimoja kila
baada ya kula na weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya kifua na majani yake
kwa bendeji kabla ya kulala. Kufungua choo: Chambua kitunguu, weka katika
maziwa na kunywa.
Kutia
nguvu na nishati:
Choma kitunguu pamoja na maganda yake halafu kichambue na ukikande katika asali
na samli,weka katika mkate wa ngano nzima kama vile sandwich. Kula wakati wa
chakula cha asubuhi na unywe maziwa nusu lita.
Kupunguza
uzito: Kwa anayetaka
kufurahia mwili wake uwe mzuri na mwepesi, kuyeyusha mafuta na kuondoa kitambi
na mwili tepwetepwe miongoni mwa wanaume na wanawake basi afuate hivi:
1. Kila siku kunywa maji ya kitunguu
maji kiasi cha kijiko kimoja kidogo unaweza kuchanganya katika juisi ya matunda
ukanywa
2.
Tembea sana na kufanya mazoezi
kwa wingi.
Imeandaliwa na GPL
0 comments:
Post a Comment