Supergro ni bidhaa maarufu
sana duniani na hasa nchi za Afrika mashariki, ni kwa namna ambayo imeweza
kumsaidia mkulima kuongeza mazao na kupunguza ghalama za kilimo hasa madawa na
mbolea. Ni bidhaa bora kutoka kampuni ya kimataifa inayoitwa GNLD {Golden
NEO-Life Diamite } International kutoka Marekani. Imesajiliwa na inafanya
biashara Tanzania kama kampuni yoyote ya kibiashara tangu April 1999.
UFUATAO NI MWONGOZO WA NAMNA
YA KUTUMIA SUPERGRO.
Mwongozo huu umeandaliwa ili
utumiwe na mkulima na sio msingi wa majadiliano ya kisayansi. Taarifa za
kisayansi zimeshatolewa na bodi ya wanasayansi washauri wa GNLD ambao ndio
nguzo ya GNLD katika utafiti, utengenezaji na uendelezaji, usimamizi na
uboreshaji wa bidhaa zote za GNLD. Supergro imesajiliwa na mkemia mkuu wa
serikali.
Taarifa hii imetolewa kama
mwongozo rahisi ili wakulima waweze kuelewa na waitumie kwa urahisi shambani.
Mwongozo huu umeandaliwa kutokana na uzoefu uliopatikana kutoka kwa wakulima
wenyewe baada ya matumizi ya muda mefu kutoka sehemu mbalimbali za Uganda,
Kenya, Iringa, Dodoma hasa Kilosa, Mbeya, Kilimanjaro, Morogoro, Mtwara, Kagera
(Nyamilamba, Kanyinya, Kanywangonga na Kishuro)
KUMBUKA
Ili kumrahisishia mkulima
matumizi ya supergro, mgavi unatakiwa kuonyesha jinsi inavyofanya kazi kwa
kwenda shambani. Toa maelezo kwa ukamilifu na isahihi na faida zake. Ikumbukwe
kwamba matokeo kwenye majedwali msingi wake ni wakulima wenyewe baada ya
matumizi sahihi ya supergro. Yanaweza kutofautiana kutoka sehemu moja na
nyingine kwa sababu ya hali ya hewa na mzingira ya eneo Fulani kwa ujumla.
Wakulima wanashauriwa kutoa ushirikiano hasa matokeo baada ya matumizi ili
ushauri mzuri uweze kutolewa na itawezesha maelezo zaidi kuandikwa na
kusambazwa kwa wengine. Kutokana na supergro ya GNLD nyuso za wakulima wengi
zinaonyesha furaha na matumaini makubwa ya maisha mazuri.
Supergro inapatikana katika
ujazo wa ml(cc)250 na lita 5. Lita 5 za supergro zinaweza kutumika kwenye eneo
la ekari 15.
KAZI ZA SUPERGRO GNLD
supergro hufanya kazi ya
kulainisha maji na kuondoa mzio wa maji. Kawaida hutiririka juu ya udongo na
majani ya mimea bila kupenya ardhini au kiasi kidogo hupenya na kuishia tabaka
la juu la udongo. Jua likiwaka maji hayo hupotea kama mvuke hewani.
Supergro ikichanganywa na
maji huweza kupenya hadi tabaka la tatu ambapo huwa kuna madini na virutubisho
vingi. Virainisho vya maji huongeza na kuboresha utendaji kazi wa madawa na
mbolea za kilimo na hutumika kama:
*Kuyeyusha hali ya
mafutamafuta hasa kwenye majani ya mimea
*Kulainisha maji na kuondoa
mzio (surface tension)
*Kutawanyisha maji kwa
ulahisi
*Ni kama gundi-Huwezesha
madawa ya kilimo aina zote kushika vizuri zaidi kwenye majani na hivyo madawa
huweza kuua wadudu badala ya wadudu kuruka pembeni kama hutatumiasupergro na
hivyo kupunguza kurudirudia kupuliza dawa, kutumia dawa kidogo kwa msimu, muda
kidogo, pesa kidogo na kuongeza mavuno.
*Kuondoa nguvu ya kushikana
kwa dawa na kuifanya ichanganyike na maji vizuri na itawanyike vizuri kwenye
maji, majani na ikae kwenye maji kwa mda mrefu bila kujitenga.
*Kuwezesha maji kupenya mpaka
tabaka la tatu la udongo. Kwa kuwa tabaka la tatu huwa gumu, mizizi hushindwa
kufyonza virutubisho na kuishia juu, supergro hulainisha tabaka la tatu na
kufanya mimea kufikia sehemu yenye virutubisho vingi na kukua vizuri.
*Kuongeza uwezo wa udongo
kutunza unyevu.
*Kuwezesha mimea kukua kwa
saizi moja na kuvunwa kwa kipindi kimoja
FAIDA ZAIDI:
*Haina sumu yoyote, ni salama
kwa binadamu na wala haiathili mazingira
*Haibadili wala kuharibu
udongo
NAMNA YA KUTUMIA
*Mililita moja (cc1) ya
supergro, changanya na lita 1 ya maji;
*Au mililita tano (cc5) za
supergro, changanya na lita 5 za maji
*Au mililita mia (cc100) za
supergro, changanya na lita 100 za maji
MAHARAGE NA SOYA:
Loweka mbegu kwa saa 4 kabla
ya kupanda kwenye mchanganyiko wa supergro na maji (rejea maelezo hapo juu
tafadhali). Loweka kiasi ambacho utatumia na kumaliza. Acha nafasi ya sentimita
30 au lula moja kila upande kati ya mbegu na mbegu.Baada ya kuota pulizia tu
wakati maharage yana majani mawili au matatu kila baada ya wiki mbili wakati wa
mvua na mara moja kwa wakati wa ukame.Kuzuia wadudu waharibifu, changanya
duducyper (mililita 15) kwenye supergro mililita 15 na maji lita 15. Pulizia
kila baada a wiki mbili mpaka maua yatakapokomaa na kudondoka yenyewe. Baadhi
ya sehemu huko Uganda wameweza kuvuna chini ya miezi miwili baada ya kupanda.
MAHINDI
Loweka mahindi kwenye
mchanganyiko wa mililita moja ya supergro na lita moja ya maji kwa siku mbili.
Panda kati ya futi (lula) moja na nusu na futi mbili kila upande wa mbegu. Weka
mbegu mbili kila shimo. Pulizia mchanganyiko wa supergro na maji (mililita 1 ya
supergro kwa lita moja ya maji) baada ya mahindi kuota yakiwa na majani mawili
hadi manne au urefu wa nusu futi. Utaendelea kupulizia mara moja kila baada ya
wiki mbili kama ni wakati wa mvua na mara moja kila baada ya wiki moja kama
kuna ukame. Pulizia kwenye majani na ardhi kuzunguka shina. Inashauriwa
kuchanganya na dawa za kuua wadudu kama kuna wadudu. Endelea kupulizia mpaka
mahindi yatakapotoa hindi. Unapotumia supergro, mahindi yana uwezo wa kutoa
hindi baada ya wiki 6 na yanakua tayari kuvunwa yakiwa mabichi baada ya
miezi 3.
MTAMA
Loweka usiku kucha. Panda
kama ilivyo katika mahindi
KARANGA
Loweka kwa saa sita tu. Panda
katika mstari kati ya nusu futi (nusu lula) kila upande na mbegu moja kila
shimo.Pulizia mchanganyiko wa supergro na maji (mililita moja kwa lita moja ya
maji) baada ya kuota mara moja kila baada ya wiki moja wakati wa ukame na
maramoja kila baada ya wiki mbili wakati wa mvua. Acha kupulizia mara
zinapoacha kutoa maua.
VIAZI VITAMU
Loweka kipande cha mbegu
(mche). Sehemu ambayo utaizika ardhini ndio iingie kwenye mchanganyiko wa
supergro (mililita kwa lita moja ya maji) kwa saa 12. Siku tatu baada ya
kupanda, pulizia mchanganyiko kama mwanzo juu ya tuta la viazi. Endelea
kupulizia mara 1 kila wiki wakati wa ukame na mara 1 kila baada ya wiki 2
wakati wa mvua. Acha kupulizia baada ya majani kutambaa na kufikia tuta la pili
yake. Kutoka kwa watumiaji wazoefu wa supergro wanasema baada ya wiki 2 hadi 3
viazi huweza kutoa viazi vichanga ukubwa wa kidole. Ni muhimu kufahamu kuwa
supergro hulainisha udongo na kuhifadhi maji kwenye matuta ya viazi wakati wa
kiangazi na viazi vinaweza kuendelea kuzaa hata mwaka mzima.
KAHAWA
Kwa mimea kama miti, pulizia
na mwagilia kuzunguka shina. Supergro inaweza kutumika kuanzia kwenye kitaru
cha miche mpaka kupandikiza uhai wote wa mibuni. Weka nusu lita ya mchanganyiko
wa supergro na maji kwenye mmea mmoja. Wakati wa mvua weka mara 2 kwa mwezi na
wakati wa kiangazi usiweke. Rudia wakati wa mvua tu. Kiasi na utaratibu kama
huu unaweza kutumika kwenye mimea kama mibuni. Unapotumia supergro, mibuni
itaanza kutoa maua kabla ya mwaka mmoja kuisha na inaweza kutoa maua mara 2 kwa
mwaka. Kwa mibuni iliyopukutika majani, ukipulizia supergro huota majani haraka
na kutoa maua haraka. Baada ya mavuno, ukipulizia supergro mibuni hutoa maua
tena. Supergro huzuia sisimizi ambao hupanda kwenye mibuni. Wakati wa kahawa
inatoa maua, pulizia supergro bila kuweka dawa yoyote ya kuua wadudu. Kwa mibuni
mikubwa, tumia lita 5 mchanganyiko wa supergro na maji katika mbuni 1 na
unaweza kutumia kwenye majani pia.
MATOKEO
Mbuni mmoja hutoa hadi kilo
20 za kahawa iliyokobolewa grade 18 NDIZI Kabla ya kupanda, loweka shina
la mgomba kwa saa 24. Baada ya kupanda weka supergro kwa kufuata utaratibu kama
uliotumika kwenye kahawa. Vilevile unaweza kutumia kwenye dawa ya kuua magugu.
VIAZI MVIRINGO-VIAZI VYA
CHIPSI
Pulizia mbegu usiku na kesho
yake panda. Baada ya kuota, pulizia kila baada ya wiki mbili mpaka vitakapoacha
kutoa maua. Shuhuda mkulima mmoja huko masaka alipanda kiloba kimoja na akavuna
viroba 15. Kwa kawaida viroba 5 hutoa viroba 15.Lakini baada ya kutumia GNLD
supergro kiloba 1 kimetoa viroba 15.
MBOGA ZA MAJANI
Hii inajumuisha nyanya,
nyanya chungu, cabbage, pilipili hoho, bilinganya, spinachi, mchicha, vitunguu
n.k
NYANYA
Loweka mbegu kwa siku 2 kabla
ya kupanda. Unaweza kupanda kwenye vitaru au moja kwa moja kwenye shimo.
Kwakuwa mbegu huwa zinashikana, ni vizuri kuziachanisha kabla ya kupanda. Mbegu
huota haraka baada ya siku 5 tu ukilinganisha na kawaida bila kutumia supergro
ambapo huota baada ya siku 14. Changanya supergro kwenye dawa zote za kupulizia
kwenye majani (mililita 1 ya supergro kwa lita 1 ya maji). Kama ni bomba la lita
20 weka mililita 20 (cc20) za supergro kufanya dawa za kuua wadudu na ukungu
kufanya kazi vizuri kwenye majani (mfano bluu kopa kwenye nyanya). Shuhuda
mkulima wa kishuro kagera Salapioni Barongo anathibitisha kuwa alivuna nyanya
ambazo hajawahi kuvuna baada ya kutumia supergro, ni mkulima wa nyanya zaidi ya
miaka 20 iliyopita. Ameshuhudia kuwa supergro inapunguza ukungu wa nyanya.
Endelea kupulizia supergro kila unapopulizia dawa mpaka nyanya zinapoacha kutoa
maua. Pia kwa kuchanganya mchanganyiko kama huo kwenye maji na kumwagilia,
supergro itapunguza kupotea kwa maji kama mvuke, na kwa kuwa maji mengi
yanazama chini hivyo kupunguza mzunguko wa kumwagilia angalau kila baada ya
siku 3. Vilevile huongeza uwezo wa nyanya kufyonza mbolea za chumvichumvi na
virutubisho vingine kutoka ardhini. Mboga za majani nyingine, fuata utaratibu
kama huo wa nyanya
ANGALIZO
Kwa mazao yafuatayo ambayo
hujichavua yenyewe unaweza kuchanganya supergro na madawa yote ya mimea na
kupulizia maua yake. Mazao hayo ni mpunga, mahindi, ngano, soya, mazao yote
jamii ya ngano, dengu, njegere, maharage, jamii yote ya pilipili, nyanya, ufuta,
bilinganya nk. Kwa mazao yote ambayo huchavuliwa na wadudu ni vizuri kufahamu
kwamba inapendekezwa usitumie madawa ya kuua wadudu wanaochazisha mimea hiyo.
Lakin supergro inaweza kutumika kwa kuwa haiui wadudu. Mazao hayo ni kama
kahawa, cocoa, apples, zabibu, alizeti, tikiti maji, matango nk
HITIMISHO
Tunapopambana kutunza ardhi
na kuhifadhi mazingira kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, supergro
imekuja wakati sahihi. Inasaidia kupunguza matumizi ya maji, kwa kuzingatia
ukweli kwamba maji yanazidi kupungua wakati huo maji ni uhai, mna kadili idadi
ya watu inavyongezeka maji yatazidi kuwa kitu adimu na kila serikali itazidi
kufuatilia kwa karibu zaidi ndio maana kuna mikakati mbalimbali ya kuhifadhi
vyanzo vya maji. Hakuna kitu kama supergro inayotumia sayansi ya asili, na GNLD
kuwasaidia wakilima kuongeza mavuno na uzalushaji. Hivyo kupambana na njaa na
umaskini Tanzania.
Somo hili limeandaliwa na :-
Francis Shija Mandwa
Mobile;- +255714138315
+255757251573
0 comments:
Post a Comment