Ads 468x60px

Featured Posts

Saturday, 11 April 2015

KIFAHAHAMU KILIMO CHA ZAO LA GILGILANI ,KUANDAA SHAMBA HADI KUVUNA NA CHANGAMOTO ZAKE.



Zao hili linalotumika kama kiungo cha chakula katika mapishi mbalimbali kama nyama, supu au mchuzi. Giligilani inafaa kulimwa wakati wowote na katika maeneo mengi ya Tanzania hususani mikoa ya Mbeya, Iringa na Arusha. Uhitaji mkubwa wa walaji pamoja na urahisi wa kuzalisha zao hili katika maeneo mbalimbali nchini, umewezesha wakulima kupata soko zuri na kujiongezea kipato kwa urahisi zaidi. 

Aina za giligilani 
Kuna aina kuu mbili za giligilani ambazo ni: Giligilani fupi na ndefu.
Aina zote hizi zinatumika kwa wingi na zinauzika katika masoko yote. 
Giligilani fupi: Aina hii ni nzuri kwa mkulima yeyote anayetaka kulima kwa lengo la kuvuna mbegu. Hii ni kwa sababu inatoa maua ikiwa fupi, inakomaa kwa haraka na mbegu zake huwa nyingi. Aina hii si nzuri sana kwa kilimo cha kuvuna majani. 
Giligilani ndefu: Hii ni aina ambayo ni bora kwa ajili ya kilimo cha kuvuna majani lakini pia mbegu zake hufaa kwa viungo. Aina hii hurefuka zaidi kabla ya kutoa maua na mbegu zake ni chache. 


Hali ya hewa 
Giligilani hustawi katika maeneo yote ya Tanzania, yenye joto lisilozidi nyuzi 20°C hadi 25°C, kiasi cha mita 1000 hadi 1800 kutoka usawa wa bahari. Pia hustawi katika maeneo yenye nyuzi joto zaidi ya 25°C kwa kulima wakati wa mvua ambapo joto huwa limepungua. Hata hivyo, mikoa ya Mbeya na Iringa ni maeneo mazuri zaidi kulima zao hili kulingana na hali ya hewa ya ubaridi katika msimu wote wa mwaka.

Udongo
Zao hili linastawi katika udongo wa aina yoyote lakini hustawi vizuri zaidi katika udongo tifutifu (Loam soil) na udongo wa kichanga (Sandy soil).

 Utayarishaji wa shamba 
Hakikisha shamba lako limelimwa vizuri, limenyeshewa vizuri na lina mbolea ya kutosha kabla ya kupanda.

 Mbolea 
Mboji inafaa zaidi kwa ajili ya kurutubisha udongo na kuongeza mavuno. Baada ya siku mbili toka kumwagiliwa, tifua tena kwa kutumia rato, kasha sawazisha vizuri kuondoa mabonde na kisha sia mbegu za giligilani.
Uoteshaji 
Uoteshaji wa giligilani hutegemea umekusudia kuvuna nini au ni aina gani ya giligilani unaotesha. 
Mfano, mkulima anaweza kuwa anakusudia kuzalisha mbegu au kuvuna majani kwa ajili ya kutumika kama kiungo. Unaweza kuotesha giligilani kwa kusia shambani moja kwa moja. 


Uoteshaji kwa ajili ya kiungo 
Endapo unakusudia kuzalisha giligilani kwa ajili ya kuvuna majani ambayo hutumika kama kiungo kwenye chakula, ni lazima uoteshe giligilani ndefu na unatakiwa kusia kama unavyosia mbegu za mchicha ila hakikisha mbegu hizo hazitarundikana mahali pamoja. 
Uoteshaji kwa ajili ya mbegu 
Endapo unakusudia kuvuna mbegu kwa ajili ya kiungo, unatakiwa kuotesha giliglani fupi ambayo mbegu zake hupandwa kwenye mashimo. 
Nafasi 
Umbali wa shimo hadi shimo liwe sentimita 10-15 na umbali kati ya mstari na mstari iwe ni sentimita 20. 
Kuota 
Giligilani huanza kuchipua kuanzia siku ya 8 hadi 15 toka kuoteshwa. Hakikisha katika siku 12 za mwanzo unamwagilia kila baada ya siku mbili, na baada ya hapo kila wiki mara mbili au tatu. Ikiwa mvua zinanyesha, hakuna haja ya kumwagilia. 

Kukomaa na kuvuna 
Giligilani hukomaa vizuri baada ya siku arobaini (mwezi na siku kumi) na hapo huwa tayari kwa kuvunwa. Kama unakusudia kuvuna majani, hakikisha unaanza kuvuna kabla ya kuanza kutoa maua au mara baada ya kufikia urefu wa sentimeta 20. Hakikisha unang’oa wakati wa asubuhi kwa kung’oa mche pamoja na mizizi yake kisha kuziosha ili kuondoa udongo wote. Baada ya hapo, funga kulingana na soko husika. Ikiwa unakusudia kuvuna mbegu, hakikisha mbegu zimekomaa kwa kubadilika rangi na kuwa kahawia. Ng’oa miche na rundika mahali pasipokuwa na maji au unyevu kwa muda wa siku saba, kisha zipige polepole hadi mbegu zote zitoke katika majani. Pepeta na fungasha tayari kwa kuuza. 

Magonjwa na udhibiti
 Giligilani tofauti na mazao mengine mara nyingi halisumbuliwi na magonjwa kabisa. Mara chache sana zao hili hushambuliwa na ukungu ambao husababishwa na wingi wa maji shambani hasa linapooteshwa wakati wa mvua kubwa na wakati wa baridi kali. Hakikisha unamwagilia kwa kiwango cha wastani huku ukiepuka kuotesha wakati wa mvua nyingi na wakati wa baridi kali. 

Wednesday, 25 March 2015

FAHAMU KUHUSU KILIMO BORA CHA MANANASI


Zao la mananasi hulimwa sana hapa nchini maeneo ya Bagamoyo, Kibaha, Geita, Mwanza, Tanga, Mtwara, Lindi na maeneo mengine. Zao hili lina kiasi kikubwa cha vitamini A na B na kiasi kidogo cha vitamini C, pia kuna madini kama potasiam, kalsiam, chuma na magnesiam

HALI YA HEWA
Manansi hustawi sana ukanda wa pwani usawa usiozini mita 900 toka usawa wa bahari ambapo kuna mvua nyingi kiasi cha milimita 1500 na unyevu wa kutosha, pia unaweza kupanda kwenye maeneo yenye mvua chache lakini kwa kutumia kilimo cha umwagiliaji, Hali ya joto ni kuanzia sentigredi 15 - 32, huwa haya stahimili baridi

UDONGO
Udongo wenye rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji ndi unaofaa kwa ajili ya kilimo cha mananasi, unaweza kutumia samadi au mbole vunde ili kuongezea rutuba ya udongo wako. 

MSIMU
Kwa ukanda wa pwani wenye mvua mbili kwa mwaka upandaji wa mananasi huanza mara baada ya mvua za kwanza kuanza, ni vizuri kupanda kwa muda mfupi ili uzaaji usipishane sana na pia kusaidia kupata mvua za kutosha kabla ya msimu kuisha.

UPANDAJI
Tumia miche ya aina moja na yenye umri sawa ili huduma zifanane na pia uzaaji uwe wa mpangilio, umbali toka mmea hadi mmea ni sentimeta 30 na mstari hadi mstari ni sentimeta 60, na umbali kila baada ya mistari miwili miwili ni sentimeta 90

Kwa ekari moja unaweza kupanda miche 25,200 na kwa hekta moja unaweza kupanda miche 44,000. ili mananasi yako yastawi vizuri basi tengeneza kama mtaro mdogo na kwenye mitaro ndio upande mananasi yako, hii husaidia kupata unyevu zaidi 

MBOLEA
Kwa wale wanaotumia mbolea za viwandani, ni vizuri kutumia NPK na DAP ambazo utaweka miezi miwili baada ya kupanda na miezi 12 baada ya kupanda baada ya hapo hautahitaji mbolea tena, lakini ni vizuri zaidi kama utatumia mbolea za asili

WADUDU
Wadudu wanaoshambulia mananasi ni aina ya mealybug ambao huondolewa kwa kupulizia dawa kama dume na karate.

Ugonjwa wa kuoza moyo wa miche unaweza kuzuiwa kwa kupiga dawa za copper oxychloride au kwa kuzamisha miche kwenye dawa za fungasi (fungicides)kabla ya kupandwa shambani

UVUNAJI
Mananasi huwa tayari kuvunwa miezi 18  mpaka 24 baada ya kupandwa kutegemeana na mbegu na matunzo ikiwemo kiasi cha mvua, mbolea na unyevu shambani, Uvunaji  hufanyika kwa kutumia visu na vibebeo maalum kuhakikisha ubora wa zao hili

SOMO MUHIMU KWA WOTE: HUU NDIO UFUGAJI WA KUKU WENYE TIJA , JIFUNZE HAPA



UFUGAJI WA KUKU

Mdau wa blog ya hii.
Wengi wetu tunafuga kuku pasi na malengo, nimekaa chini na nikaona uchoyo ni jambo moja baya sana linalotuumiza sana watanzania katika maendeleo ya kila jambo. (Hasa uchoyo wa mawazo, tunalaumu mno hatutoi mawazo yenye tija)
Leo naongelea kuhusu ufugaji wa kuku, hasa kuku wa kienyeji ufugaji wenye tija.


Kuku hawa ni rahisi sana kuwafuga lakini ni wagumu sana kama hutokuwa makini na kama huna malengo na ufugaji wako.  Wengi wetu tunafuga tu huku tukiwa na matarajio makubwa ya mafanikio.  Unajidanganya ndugu yangu, huwezi kutegemea kitu ambacho hukipendi na hukigharamii.  Kuku wanatakiwa kula, kuku wanatakiwa kunywa, kuku wanatakiwa kupata huduma za dawa, kuku wanataka kulala sehemu nzuri na safi, yenye hewa, wanapopendwa, wanapojaliwa, kuku wanahisia kama viumbe wengine huwa wanapenda wakiwa na shida uwaangalie kama unavyoangalia kitu kingine chenye uhai na uwasaidie, lakini ukiwa mkaidi kwao nao watakuletea ukaidi.  Haya ni maneno huwa naambiwa na mama yangu mzazi bi Paulina, huwa anawaangalia kuku wangu na anasema hawa kuku wana shida lakini huwaelewi, sasa nimeanza kumuelewa na ndio maana nataka nikupe elimu hii nawe uweze kufaidika.

ONDOA UCHOYO KWANZA

Kama umeamua kufuga kweli basi fanya haya, usiwe bahili wa muda kwa kuku wako, usiwe bahili wa vitu vifuatavyo;
a.       Fedha za kununulia chakula
b.      Fedha za dawa na daktari
c.       Fedha kwaajili ya kununua mboga za majani au ufanye kilimo cha mboga za majani ili uwalishe
d.      Fedha kwaajili ya ulinzi wa kuku wako
e.       Fedha kwa mtunzaji wa kuku wako
f.       Fedha za usafirishaji kwenda kwa wateja wako, au katika manunuzi ya kuku wageni




Lakini kuna jambo kubwa zaidi, umoja kati yako wewe na wafugaji wenzako.
Na hii leo ndio mada yangu kuu.
Umoja wa wafugaji katika eneo hilo ulilopo, ndio nguzo kuu ya kupata kipato kikubwa zaidi na kuwa na soko kubwa zaidi mwaka mzima na miaka yote na hakuna mtu anatakayekosa huduma ya kuuziwa kuku au mayai katika eneo lenu ikiwa mtakuwa wamoja kwa ufugaji wa kuku.

LENGO MOJA NA MOYO MMOJA
Ni vigumu sana kwa watu zaidi ya 100 kuwa na lengo moja kwa miaka zaidi ya 10, lakini kama mtaamua na mkaona faida yake inawezekana tena kwa 100%.  Naongea haya kwa kuwa naona kabisa ili ufanikiwe kuwa kama unataka kuku 10,000 kwa kipindi kifupi ni ngumu lakini wafugaji 30 mkiunda kikundi na mkachangishana labda shilingi 500,000 kwa kila mmoja mtapata shilingi za kitanzania 15,000,000.  Mkiamua sasa mjenge banda la shilingi 3,000,000 zitabaki 12,000,000. Na mkinunua chakula cha shilingi 3,000,000 zitabaki milioni 9,000,000.  Wengi wa wauzaji wa kuku huuza kuku waliochanjwa hivyo unaweza kukaa na kuku wale kwa miezi mitatu zaidi wakiwa wako vizuri bila kuugua. Nunueni kuku kwa shilingi 1,600, leo nakupa siri kama ulikuwa hujui nipigie simu nitakuambia vizuri wapi pa kununulia na utashangaa utakuja kuwa na kuku hadi ulie. Katika milioni 9,000,000 zilizobaki nunua kuku wa shilingi 5,000,000 kwa kila mmoja kumnunua kwa shilingi 1,600 utapata kuku wangapi? 

Utapata kuku 3,125.  Kuku hawa utawanunua wakiwa na umri wa miezi mitatu na nusu, hivyo utawakuza kwa miezi miwili na nusu wataanza kutaga.  Lakini kama mtataka kuwa na kuku wengi zaidi kwa muda wa miezi 6 mnaweza kuwa kundi lenu la watu 30 mkawa mnachangishana 200,000 kila mmoja ina maana kila mwezi mtapata shilingi 6,000,000 x 6 = 36,000,000.
36,000,000/1,600 = 22,500
Kundi litapata kuku 22,500 ina maana kama kuku mmoja baada ya miezi minne atauza kwa shilingi 10,000 kwa kuku 22,500 kikundi kitapata shilingi 225,000,000.
Kwa maana hii kikundi kitakuwa kimepata faida ya shilingi;
225,000,000 – 36,000,000 = 224,964,000
224,964,000 – 50,000,000 = 174,964,000
Hiyo hesabu ni makadirio na matumizi ya kilichopatikana ilitumika 36,000,000 kununua kuku 22,500 wakauzwa kwa shilingi 10,000 kwa kila mmoja ikapatikana shilingi 225,000,000 tunatoa fedha ya manunuzi iliyokuwa shilingi 36,000,000 hivyo itabaki shilingi 224,964,000 katika pato hilo la 224,964,000 toa 50,000,000 ya vyakula, maji, mlinzi, mhudumu, umeme na maji utabaki na shilingi 174,964,000 (weka hasara ya kuku wengine kufa) faida itakuwa 100,000,000
Hii inaweza kufanya kila mwanachama wa kikundi akawa na faida ya shilingi 3,333,333.30 ambapo mkiamua kujiwekea malengo ya kuuza kuku kwa mizunguko 1,000 kila mwanakikundi atakuwa na faida ya shilingi 333,333,300 na hii inawezekana sana kama kundi lina nia na linaupeo na si kulalamika kila wakati.  Tatizo letu watanzania ni walalamishi sana sio wote ila asilimia kubwa ni walalamishi.  Nina hakika kundi hili linaweza kujikwamua kwa kuku tu bila kujichanganya na jambo lingine.  Kundi likijipa miaka mitano ya kufanya biashara hii kwa nguvu na nia itakuwa mfano wa kuigwa.
Kumbuka kuna kundi la kwanza la kuku 3,125 ambapo kuna shilingi 4,000,000 ilibaki benki kama kilinda benki, kikundi hiki kwa mahesabu yale yale kina uwezo wa kutengeneza shilingi  na shilingi za mamilioni.  Ila sasa huku itazitengeneza kwa kuzalisha mayai ya kuku wa kienyeji.

MAYAI YA KIENYEJI
Ikiwa kuku  3,125 majogoo yatakuwa 1,125 na majike 2,000 basi una uhakika wa kuwa na trei 66 kwa siku.  Chukulia mfano siku 7 za wiki unachukua mayai manne tu kwa wiki utapata mayai 16 kwa kuku hii inamaana utapata mayai 32,000 kwa mwezi ambayo ni trei 1,066.  Trei moja ya mayai ikiuzwa shilingi 12,000.

1,066 x 12,000 = 12,792,000 kwa mwezi
12,792,000 x 12 = 153,504,000 kwa mwaka
Kwa maana hiyo mayai yanaweza kuingiza shilingi 153,504,000 ukitoa gharama za usafirishaji na mhudumu mnaweza ingiza 100,000,000 kwa kuuza mayai ya kienyeji pekee.

Kwanini tusijiunge tukafanya shughuli hii?
Unasubiri nini?
Unataka kuona nimetajirika kwanza ndio na wewe uhamasike?
Usiwe mchoyo njoo tujiunge tukuze kipato kwa biashara hii niliyokupa sasa hivi


MBOLEA  YA KUKU
Kinyesi cha kuku ni mbolea nzuri sana kwa wakulima, kwa idadi ya kuku iliyopo katika kikundi na inayoendelea kuwepo kila mfuko wa mbolea ya kuku inauzwa shilingi 2,000.  Ikiwa kikundi kitakuwa na mifuko isiyopungua 2,000 basi kikundi hakitakosa shilingi 4,000,000 iliyotokana na mbolea.



Maoni yako ni muhimu sana 

MUHIMU KWA WAFUGAJI NA WAKULIMA: FAHAMU BIASHARA NZURI YA BATA MZINGA, SOMA HAPA



BATAMZINGA

Bata Mzinga ni biashara nzuri sana ambayo watu wengi hatuitilii maanani sana.  Soko la Bata Mzinga ni kubwa sana katika Supermarkets.

             
Wengi watahoji nitafugia wapi! Hautakuwa una shida ya hela ndugu yangu, lakini sikulaumu sana kwa kuwa mfumo wa sisi hasa watanzania ni kuajiriwa, na ajira zetu hizi za kupata mwisho wa mwezi kiasi kidogo cha hela na kuridhika, huwa kinatudanganya sana.  Wengi wetu hujiingiza katika makundi ya udanganyifu kwa kuwa tunatafuta kipato cha ziada kwa njia isiyo halali, na mwisho wa siku ajira zetu sasa zina dhambi, dhambi ya rushwa, kutokuaminika, kuharibiana ajira.  Hii yote ni dhambi tu, hatutaki kushirikiana ili kuweza kufanya kazi kwa bidii na kukuza kipato chetu na kufanya kazi za umma kwa maslahi binafsi, na maslahi ya umma.
Sio mada yangu hii leo lakini naomba tujue baadhi ya sababu zinazojenga ukanjanja kazini.  Hatujipangi kikamilifu, tunacheza na majukwaa (tunataka kuonekana na jamii tuna uwezo kumbe si kweli)
Bata Mzinga ni bata anayefugwa nyumbani, na ana uwezo wa kukua hadi kufikia kilo 15, ni
pambo la nyumba pia.

Kwanini namuongelea Bata Mzinga leo, nimegundua kila ninapoenda katika Super Markets kubwa nakuta nyama ya bata hawa inauzwa na tena bei kubwa tu, mfano mimi nilinunua kifaranga cha bata mzinga kwa shilingi 25,000 walikuwa watano ambayo ni sawa na shilingi 125,000.
Kwa wale wanaojua kilo moja ya bata mzinga inauzwa kuanzia shilingi 10,000 na bata mzinga ana kilo 15 ni sawa na shilingi 150,000 hivi huoni kuwa huyu muuzaji wa kilo moja moja anafaida kubwa sana kuliko wewe mkulima?
Bata mzinga mmoja mwenye kilo 12 kwa jike na kilo 15 kwa dume anauzwa hivi;
Bata mzinga jike ni shilingi 60,000
Bata mzinga dume ni shilingi 70,000
Mfano una bata mzinga 2,000, majike 1,000 na madume 1,000 unajua utakuwa una miliki shilingi ngapi?
Ukiwa na majike 1,000 wenye thamani ya shilingi 60,000 = 60,000,000
Ukiwa na madume 1,000 wenye thamani ya shilingi 70,000 = 70,000,000
                                                                                                                       
Mfano ukijiingiza katika biashara hii kwa kununua bata mzinga wadogo 40 kwa shilingi 25,000 kwa kila mmoja unaweza kupata majike 25 na madume 15 kwanza ili uanze kutengeneza kizazi cha kufuga kwanza.  Chukulia mfano jike moja likitotoa vifaranga 10 x 25 = 250.  Fanya kila bata mzinga atotoe mizunguko mitano itakuwa 250 x 5 = 1,250

Sasa chukua hao watoto 1,250 nao wawe madume nusu na majike nusu 625 x 10 = 6,250.  Chukua idadi ya kwanza 40 + 250 + 1,250 + 6,250 = 7,790 unaona wanavyoongezeka kutoka 40 hadi sasa una bata mzinga 7,790 tayari hapa wewe ni milionea hizi ni sawa na shilingi 467,400,000 unazo ndani.
Bata mzinga 7,790 ukiwagawa madume na majike nusu kwa nusu utapata majike 3,895 chukua kila bata mzinga atotoe vifaranga 10 kila mmoja utapata bata mzinga 38,950

UUZAJI VIFARANGA
Hawa bata mzinga 38,950 unaweza kuuza kama vifaranga, na kila kifaranga utakiuza kwa shilingi 25,000.  38,950 x 25,000 = 973,750,000 hii ni fedha taslimu utaipata kwa kuuza vifaranga.


 
Katika miaka kumi ya ufugaji wako wa bata mzinga unaweza kujikuta unakuwa bilionea kama ukiwa makini na mwenye nia kweli ya kuzitafuta pesa kwa kuwafuga hawa bata. 
Leo tumeanza na bata mzinga 40 lakini tunamaliza na bata mzinga 46,740 wastani wa bata mzinga 50,000.
Kazi yangu ni kukupa changamoto mdau mwenzangu katika kutengeneza maisha ya ufugaji na fedha.  Unaweza kustaafu kazi ya kuajiriwa lakini ukaanza ufugaji na ukatengeneza hela nyingi zaidi, usikate tama.  Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, alianza madaraka mwaka 2005 jana tu tulimpigia kura kwa shangwe na vigelegele, kumbuka 2010 tena tumempigia kura na sasa amebakiza mwaka mmoja tu wa madaraka yake, je huoni kuwa jana tu imeshageuka leo? Hujachelewa bado kwa mwaka huu wa madaraka yake na mwezi huu Januari, 2014 badilika anza ufugaji nenda na malengo kama haya, nakuhakikishia nitakutafutia masoko pia, na nitakutangaza kwa moyo wangu wote. Sijui atakayenisaidia mbele ya safari.  Ila wewe utakayefuata haya ninayokuambia na ukafanikiwa usinisahau katika ufalme wako, hata kama sitakuwepo basi waangalie hata wanangu.

Ushauri wangu kwako usitake makubwa haraka nimekupa mfano wa Raisi wan chi ili uone kuwa miaka 10 ni mingi kuitaja, lakini ni michache ukibung’aa huku unangoja maisha bora na elimu yako unapanda jukwaani unalalamika pamoja na asiyena elimu, ni wakati sasa wakutoa vilivyo kichwani na kuviweka katika maandishi na vifanyiwe kazi.
Tuwasiliane kwa kupeana mawazo
Maoni yako ni Muhimu sana

Friday, 20 March 2015

SOMO MUHIMU KWA WOTE: PIGANA NA UMASIKINI KWA KUTUMIA SUPERGRO KATIKA KILIMO NA MAZAO MBALIMBALI.






Supergro ni bidhaa maarufu sana duniani na hasa nchi za Afrika mashariki, ni kwa namna ambayo imeweza kumsaidia mkulima kuongeza mazao na kupunguza ghalama za kilimo hasa madawa na mbolea. Ni bidhaa bora kutoka kampuni ya kimataifa inayoitwa GNLD {Golden NEO-Life Diamite } International kutoka Marekani. Imesajiliwa na inafanya biashara Tanzania kama kampuni yoyote ya kibiashara tangu April 1999.

UFUATAO NI MWONGOZO WA NAMNA YA KUTUMIA SUPERGRO.

Mwongozo huu umeandaliwa ili utumiwe na mkulima na sio msingi wa majadiliano ya kisayansi. Taarifa za kisayansi zimeshatolewa na bodi ya wanasayansi washauri wa GNLD ambao ndio nguzo ya GNLD katika utafiti, utengenezaji na uendelezaji, usimamizi na uboreshaji wa bidhaa zote za GNLD. Supergro imesajiliwa na mkemia mkuu wa serikali.

Taarifa hii imetolewa kama mwongozo rahisi ili wakulima waweze kuelewa na waitumie kwa urahisi shambani. Mwongozo huu umeandaliwa kutokana na uzoefu uliopatikana kutoka kwa wakulima wenyewe baada ya matumizi ya muda mefu kutoka sehemu mbalimbali za Uganda, Kenya, Iringa, Dodoma hasa Kilosa, Mbeya, Kilimanjaro, Morogoro, Mtwara, Kagera (Nyamilamba, Kanyinya, Kanywangonga na Kishuro)

KUMBUKA

Ili kumrahisishia mkulima matumizi ya supergro, mgavi unatakiwa kuonyesha jinsi inavyofanya kazi kwa kwenda shambani. Toa maelezo kwa ukamilifu na isahihi na faida zake. Ikumbukwe kwamba matokeo kwenye  majedwali msingi wake ni wakulima wenyewe baada ya matumizi sahihi ya supergro.  Yanaweza kutofautiana kutoka sehemu moja na nyingine kwa sababu ya hali ya hewa na mzingira ya eneo Fulani kwa ujumla. Wakulima wanashauriwa kutoa ushirikiano hasa matokeo baada ya matumizi ili ushauri mzuri uweze kutolewa na itawezesha maelezo zaidi kuandikwa na kusambazwa kwa wengine. Kutokana na supergro ya GNLD nyuso za wakulima wengi zinaonyesha furaha na matumaini makubwa ya maisha mazuri.

Supergro inapatikana katika ujazo wa ml(cc)250 na lita 5. Lita 5 za supergro zinaweza kutumika kwenye eneo la ekari 15.

KAZI ZA SUPERGRO GNLD

supergro hufanya kazi ya kulainisha maji na kuondoa mzio wa maji. Kawaida hutiririka juu ya udongo na majani ya mimea bila kupenya ardhini au kiasi kidogo hupenya na kuishia tabaka la juu la udongo. Jua likiwaka maji hayo hupotea kama mvuke hewani.

Supergro ikichanganywa na maji huweza kupenya hadi tabaka la tatu ambapo huwa kuna madini na virutubisho vingi. Virainisho vya maji huongeza na kuboresha utendaji kazi wa madawa na mbolea za kilimo na hutumika kama:

*Kuyeyusha hali ya mafutamafuta hasa kwenye majani ya mimea

*Kulainisha maji na kuondoa mzio (surface tension)

*Kutawanyisha maji kwa ulahisi

*Ni kama gundi-Huwezesha madawa ya kilimo aina zote kushika vizuri zaidi kwenye majani na hivyo madawa huweza kuua wadudu badala ya wadudu kuruka pembeni kama hutatumiasupergro na hivyo kupunguza kurudirudia kupuliza dawa, kutumia dawa kidogo kwa msimu, muda kidogo, pesa kidogo na kuongeza mavuno.

*Kuondoa nguvu ya kushikana kwa dawa na kuifanya ichanganyike na maji vizuri na itawanyike vizuri kwenye maji, majani na ikae kwenye maji kwa mda mrefu bila kujitenga.

*Kuwezesha maji kupenya mpaka tabaka la tatu la udongo. Kwa kuwa tabaka la tatu huwa gumu, mizizi hushindwa kufyonza virutubisho na kuishia juu, supergro hulainisha tabaka la tatu na kufanya mimea kufikia sehemu yenye virutubisho vingi na kukua vizuri.

*Kuongeza uwezo wa udongo kutunza unyevu.

*Kuwezesha mimea kukua kwa saizi moja na kuvunwa kwa kipindi kimoja

UMUHIMU, FAIDA NA MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU MAJI



MARADHI YANAYOTIBIWA NA KITUNGUU MAJI

Pumu: Changanya juisi ya kitunguu maji na asali halafu kunywa kiasi cha kikombe kimoja, asubuhi na jioni. Endelea hivyo kwa muda wa mwezi mmoja.

Uvimbe wa mapafu (Pneumonia): Weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya kifua na mgongo pamoja na kufunga kwa kitambaa, fanya hivyo kila siku kabla ya kulala. 

Maradhi ya kinafsi: Chemsha kitunguu na maganda yake, baadae mgonjwa wa kinafsi ale, au chukua juisi ya kitunguu maji na juisi ya saladi (lettuce) na kijiko kimoja cha asali changanya vyote ndani ya blenda saga na kisha unywe. 

Saratani (Cancer): Kausha maganda ya kitunguumaji kwenye jua, yasage na kiasi cha magamba hayo chukua magamba ya muoka (muoki, maloni, oak) halafu yakande katika asali na chukua na uchanganye katika juisi ya karoti (carrot) na unywe kiasi ya kijiko kimoja kwa muda wa mwezi mzima mfululizo,na baadae uvute moshi wa kitunguu maji kabla ya kulala.

Vidonda ya saratani: Chukua juisi ya kitunguumaji kiasi cha kikombe,chukua na kiota (kiwawi, nettle) kamua majani yake kiasi cha kijiko kimoja na ongezea juisi ya kitunguu na halafu chukua hina iponde ndani yake ili ipate kuwa marhamu inayopakwa katika vidonda; fanya hivo kila siku pamoja na kunywa juisi ya kitunguu maji iliyochanganywa na juisi ya kiota kijiko kimoja kidogo na baada ya hapo kunywa kikombe kimoja cha maziwa. 

Mvilio wa damu (Bruise): Changanya juisi ya kitunguu maji pamoja na kiasi cha mafuta ya kafuri, sugua mahali palipo na  mvilio asubuhi na jioni. 

Majipu: Saga kitunguu maji na kikaange katika mafuta ya zaituni bila ya kuwa rangi ya manjano, paka kama marhamu na funga bendeji juu yake. Kila siku ukibadilisha pamoja na kusafisha utokaji wa usaha umalizike, halafu utakuwa ukitumia habasouda. 

Chunusi: Chukua kitunguu maji kisha ukisage, halafu ukikande katika unga wa ngano nzima, changanya na yai pamoja na mafuta ya simsim(ufuta) na upake usoni asubuhi na jioni pamoja na kula kitunguu kwa sana. 

Ukurutu (Eczema): Chukua juisi ya kitunguu na nanaa (mint) vipimo sawa,tengeneza kama krimu (cream) na ujipake baadae pangusa ukurutu kwa maji ya siki nyepesi, rudia kila siku pamoja na kujiepusha na kila kinachochea hisia. Kula matunda,mboga na asali kwa wingi.

Saratani ya ngozi: Chukua juisi ya kitunguu maji, uwatu uliosagwa na salfa manjano kiasi cha robo kijiko kidogo; tengeneza marhamu jipake kila siku. Baada ya kuosha jioni jipake mafuta ya zaituni endelea hivyo kwa muda wa wiki. 

Mgonjwa wa figo na vijiwe: Chukua kitunguu bila kukichambua, weka na  mbegu ya tende baada ya kuichoma kama vile buni na kuisaga; halafu kila siku kula kimoja kula kimoja kwa muda wa wiki. 

Kikohozi kwa wakubwa na wadogo: Saga kitunguu kitie ndani ya kikombe cha asali; acha kwa muda wa saa tatu (3) kisha uisafishe. Kula kiasi cha kijiko kimoja kila baada ya chakula. 

Kisukari (Diabetes): Kila siku kula kitunguu. Sukari itashuka na baadae kula mzizi wa kabichi (cabbage).

Maradhi ya macho: Chukua maji ya kitunguu na asali vipimo sawa halafu ujipake jichoni (kama unavyojipaka wanja) , (dawa hii naamini ni dawa bora kwa maradhi ya macho yote nakuambuka marehemu bibi yangu alikuwa akiwatibu wagonjwa wenye mtoto wa jicho kwa kutumia dawa hii) jipakae jichoni kwa kutumia glass rod au kama huna kifaa hicho unaweza kutumia nyoya la kuku au ndege yoyote.

Kikohozi: Chemsha maji ya kitunguu maji na asali kunywa kijiko kimoja kila baada ya kula na weka kibandiko cha kitunguu maji juu ya kifua na majani yake kwa bendeji kabla ya kulala. Kufungua choo: Chambua kitunguu, weka katika maziwa na kunywa.



Kutia nguvu na nishati: Choma kitunguu pamoja na maganda yake halafu kichambue na ukikande katika asali na samli,weka katika mkate wa ngano nzima kama vile sandwich. Kula wakati wa chakula cha asubuhi na unywe maziwa nusu lita.
Kupunguza uzito: Kwa anayetaka kufurahia mwili wake uwe mzuri na mwepesi, kuyeyusha mafuta na kuondoa kitambi na mwili tepwetepwe miongoni mwa wanaume na wanawake basi afuate hivi:
1.  Kila siku kunywa maji ya kitunguu maji kiasi cha kijiko kimoja kidogo unaweza kuchanganya katika juisi ya matunda ukanywa
2.   Tembea sana na kufanya mazoezi kwa wingi.

Imeandaliwa na GPL