Ilikuwa
ni mwaka 2013 katika maonesho ya nane nane mkoani Dodoma (Nzuguni) kwenye banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ambapo
nilibahatika kuona kitu kipya katika macho yangu.
Wakulima
wengi katika nchi yetu huwa wanalalamikia miundo mbinu, lakini wana sahau kuwa
wao wenyewe wanatakiwa kuwa wabunifu wa mambo mengi badala ya kulaumu na
kulalamikia vitu ambavyo wakikaa na kutafakari wanaweza kucheka wenyewe.
Katika
mada yangu leo naandika juu ya jokofu la asili ambalo linatengenezwa kwa kutumia
miti, mkaa, nyasi, na wavu. Ni banda
ambalo linaweza kuhifadhi mazao mabichi kwa muda wa majuma mawili hadi mwezi
mmoja wakati wakiendelea kutafuta masoko.
Hakuna wadudu, pia mazao hayanyauki wala kupoteza ladha yake.
Ndani
ya banda hilo kunakuwa na ubaridi mwingi tu wa kutosha kuhifadhi matunda,
mbogamboga pamoja na vyakula vilivyo fresh kutoka shamba.
Ni
kibanda kilichojengwa kwa nguzo za miti na kuwekwa wavu wa kawaida tu.
Kisha katikati ya kuta za wavu, ukajazwa mkaa huu wa kawaida utumikao kwa
kupikia majumbani kwetu. Huu mkaa unalowanishwa kwa maji kila siku au
kama maji ni ya shida baada ya siku moja. Mkulima ukiwa na banda hili
huna hofu ya kuharibikiwa na mazao kwa muda wa mwezi mmoja wakati ukifanya
mauzo yako au kutafuta masoko. Kwa kuwa
hatuna kasumba ya kuandika mradi kabla ya kulima, na hata kama utakuwa na
andiko la mradi basi banda hili ni moja ya vitendea kazi utakavyotakiwa kuwa
navyo. Wafugaji na wakulima tuwe
watafiti na wabunifu wa shughuli zetu.
Pendelea kujiunga na vikundi kama mfumata ili uweze kupata mawazo mapya.
2 comments:
Ni mkombozi na pia ni njia rahisi ya kuweza kumpa mkulima tafakuri ya nn afanye na wapi apeleke mzigo wake kabla haujaharibika. Njia safi ya ubunifu hii kwa kweli
Umeongea ya kweli kabisa ndugu Salehe Johar
Post a Comment